Rais IDRIS DEBY wa Chad amesema kikundi cha Boko Haram kimepata kamanda mpya ambaye yuko tayari kwa mazungumzo na serikali mpya ya Nigeria kumaliza maasi ya miaka sita ya kikundi hicho.
Taarifa hiyo ya Bwana DEBY iliyotangazwa na radio ya Chad imeongeza uvumi kwamba
kiongozi wa kikundi hicho Bwana ABUBAKAE SHEKAU alikuwa amekufa.
Rais huyo wa Chad ambaye mwaka uliopita alijaribu kufanya mazungumzo yaliyoshindikana na kikundi cha Boko Haram alisema kiongozi mpya wa kikundi hicho ni mtu anayejulikana kwa jina la MAHAMAT DAOUD.
Aidha amesema kikosi cha kanda cha mataifa matano kitasambazwa siku chache zijazo na
kubashiri kuwa kitakiangamiza kikundi hicho cha Boko Haram kufikia mwishoni mwa mwaka
huu.
Home
Kimataifa
Rais wa chad asema Boko haram wapata kamanda mpya atakaye kaa na Buhari kumaliza maasi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment