Image
Image

Hukumu ya kifo iliyotolewa kwa mfungwa mmoja aliyemuua polisi miaka 6 iliyopita katika jimbo la Texas yatekelezwa.


Miaka 6 iliyopita, Daniel Lee Lopez aliwahi kufungwa gerezani na kupewa hukumu ya kifo kwa madai ya kumuua polisi katika jimbo la Texas nchini Marekani.

Mfungwa huyo mwenye umri wa miaka 27, ameripotiwa kuuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu kama utekelezaji wa hukumu ya kifo aliyopewa.

Lopez aliitaka mahakama kusogeza karibu zaidi tarehe ya hukumu ya kifo wiki iliyopita na kusababisha mawakili kuwasilisha ombi la kukata rufaa kwa kudai kwamba mfungwa huyo alikuwa na matatizo ya kiakili.

Mahakama kuu ya Marekani ilifutilia mbali ombi hilo la mawakili la kutaka kukata rufaa.

Mnamo mwezi Machi mwaka 2009, Lopez alimuua afisa mmoja wa polisi kwa jina la Stuart Alexander kwa kumgonga kwa gari, wakati alipokuwa akijaribu kutoroka polisi barabarani.

Lopez amekuwa mtu wa kumi kutekelezewa hukumu ya kifo mwaka huu katika jimbo la Texas nchini Marekani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment