Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana BAN KI-MOON amemfukuza kazini mkuu wa majeshi ya kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na tuhuma za wanajeshi wake kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji wa ngono kwa watoto.
Bwana BAN amewaambia waandishi wa habari kwamba kutokana na tuhuma hizo alimwomba Bwana BABACAR GAYE ajiuzulu kwani alikasirishwa na kuabishwa na vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji vinavyodaiwa kufanywa na wanajeshi hao wa kulinda amani.
Siku moja kabla ya kujiuzulu kwa Bwana GAYE Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za
Binadamu Amnesty International lilidai msichana wa miaka 12 kubakwa na mwanajeshi wa
kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa chenye wanajeshi 10,000 wa kulinda amani huko Jamhuri ya
Afrika ya Kati pia inadaiwa askari wake wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya
udhalilishaji kingono kwa watoto wa mitaani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment