(BASATA) kwa kipindi cha mwaka mmoja amekanusha habari zinazosambazwa mitandaoni kuwa amepata ajali.
Hapo jana katika mitandao ya kijamii kuna taarifa ilikuwa ikisambazwa ambayo ilikuwa inasema Shilole amepata ajali na kupoteza maisha alipokuwa akisafiri, jambo ambalo yeye mwenyewe ameibuka na kulazimika kukanusha taarifa hizo.
Shilole amekiri wazi kuwa ana matatizo mengi yanayomkabili kwa sasa ila amewataka watanzania wazidi kuombeana uzima na mambo mazuri, na si kuombeana umauti na mambo mabaya mabaya kama wanavyofanya sasa.
"Hellow Africa na mashabiki wangu mimi ni mzima wa afya namshukuru Mungu na nipo nyumbani muda huu, sijapata ajali wala sijasafiri ni uzushi wa watu tu. Nawapenda sana tuombeane uzima na si umauti na ninajua nimekumbwa na matatizo mengi ila sio kwa kuzushiwa kifo inauma sana, " Shilole aliandika ujumbe huo kupitia Instagram yake.
Mbali na hilo Shilole amezidi kudhihirisha mapenzi yake kwa Nuh Mziwanda yapo palepale baada ya kupost picha wakiwa pamoja na kisha kuandika maneno ambayo yanasomeka hivi, “Mimi siachani nawe na nitakupenda zaidi!,” licha ya kuvujishwa sauti ambayo inaonyesha mpenzi wake huyo alikuwa akimtaka kimapenzi msanii wa Bongo movie Wema Sepetu.
Wasanii hao wapenzi kwa sasa wanatamba na wimbo wao wa pamoja ambao unafahamika kama 'Ganda la Ndizi'.

0 comments:
Post a Comment