Hali hiyo imeelezwa kuwa ndiyo
sababu kubwa inayochangia pia Tanzania kuwa na wazee wengi masikini.
Katika kikao kilichoshirikisha
wazee,wafanyabiashara,taasisi za fedha na serikali kutoka wilaya sita za Mkoa
wa Njombe, ajenda kubwa ni kutafuta ufumbuzi wa kuhakikisha wazee wanatambuliwa
na taasisi za fedha na kukopesheka.
Shirika linalohudumia wazee la
Padi Tanzania, kwa miaka 15 limekuwa likifanya kazi ya kuwakopesha wazee katika
mikoa ya Ruvuma na Njombe, na limetoa vyeti vya usajili kwa vikundi 24 vyenye
wazee 1,500 Mkoani Njombe, lengo likiwa
ni kuendelea kufungua mianya ya taasisi za fedha na wafanyabiashara kuwatambua
wazee na kuwapa mikopo.
Kwa upande wao wazee wa Njombe
wanasema ifike wakati fikra za kwamba wazee hawakopesheki zikome, na kwamba
wapo tayari kukopa na ni warejeshaji wazuri wa mikopo kuliko inavyofikirika na
vyombo vingi vya fedha kuwa wamefikia ukomo wa kuishi.
0 comments:
Post a Comment