Kamishna wa Polisi MOHAMMED
MPINGA ametoa agizo hilo wakati akizungumza na waendesha pikipiki hizo maarufu
kama boda boda wa jiji la Tanga wakati wa ufungaji wa mafunzo ya elimu ya
usalama barabarani kwa ajili ya kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikipoteza
maisha ya Watanzania kwa sababu ya kushindwa kuzingatia sheria za usalama
barabarani
Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi
cha Usalama Barabarani mkoani Tanga Mrakibu Mwandamizi wa Polisi ABDI ISSANGO
amesema katika kipindi cha kuanzia mwaka 2014 hadi sasa jeshi hilo limeshatoa
mafunzo kwa waendesha pikipiki zaidi ya 340 katika jiji la Tanga, idadi ambayo
ni kubwa na imesaidia kupunguza ajali za barabarani
Naye Ofisa Habari waKkampuni ya
Bia Tanzania ambayo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania iliratibu
zoezi la utoaji wa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki za
BODABODA DORISI MALULU amewataka wasafirishaji wa pikipiki kuwa mabalozi wazuri
kwa wenzao ambao hawajapata elimu hiyo, ili waweze kunufaika.
0 comments:
Post a Comment