Kupitia taarifa ya kamanda wa
polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova amesema kuwa maandamano ya kusindikizwa mgombea urais wa
CHADEMA yana kibali cha kuanzia makao makuu ya kinondoni ilipo CHADEMA hadi NEC
na kurudi,lakini sikama inavyoelezwa kuwa maandamano hayo yataanzia Ofisi za
CUF ilala buguruni na kupitia NCCR hivyo kwenda NEC kuchukua fomu suala hilo hawalitambui
na hawalijui kwani huenda likasababisha fujo na mzunguko usio wa lazima na
kuweka foleni maeneo ya Dar es Salaam na viunga vyake.
Katika kuliweka sawa suala hili
moja kwa moja tulimtafuta mwenyekiti mwenza wa UKAWA ambaye pia ni mwenyekiti
wa CHADEMA Freeman Mbowe kufafanua hili ambapo amesema kuwa wao hawana taarifa
yeyote ya mabadiliko ya kumsindikiza mgombea urais wa chama chao kwenda
kuchukua fomu ofisi za NEC leo hii.
Pia Mh.Mbowe ameongeza kwa kusema
kuwa dhamira yao ya kumsindikiza mgombea urais kupitia CHADEMA na UKAWA
kiujumla ipo palepale kwani suala la kuanzia CUF ama NCCR sijambo la kushangaa
kwa kuwa sehemu hizo zote ni umoja wao ndani ya UKAWA.
Taarifa ya jeshi la Polisi,kukubali maandamano.
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limeona ni Busara kuruhusu maandamano ya wafuasi wa UKAWA kumsindikiza mgombea wao ili kuleta mahusiano mazuri kati ya Vyama hivyo na Jeshi la Polisi. Jeshi la polisi litasindikiza maandamano hayo. Aidha kamanda Kova amesema hayo si maandamo bali ni usindikizaji wa mgombea huyo wa UKAWA.

0 comments:
Post a Comment