Tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa
Mheshimiwa Makamu wa Rais hajapanga tukio lo lote la kukutana na waandishi wa
habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na
Chama Cha Mapinduzi.
Tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye
tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa
kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta
taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyotambulika.
Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
10/8/2015.
0 comments:
Post a Comment