Chama cha ACT wazalendo kimewataka watanzania
kutodanganyika na sifa wanazo vikwa baadhi ya wagombea wa urais katika kipindi
hiki cha kuelekea uchaguzi kwani baadhi yao wameshindwa kudhibiti wizi na
ubadhirifu wa mali ya umma katika nyadhifa walizokuwa nazo hivyo hawafai kupewa
dhamana kubwa ya kuiongoza nchi kwakuwa hakuna jipya watakaloleta zaidi ya
kuendeleza uporaji wa mali ya umma
Akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya
Mwembetogwa mjini Iringa kiongozi wa chama hicho Bwana.Zitto Zuberi Kabwe
amesema kumekuwa na maneno mengi ya kuwapamba baadhi ya wagombea wa urais hasa
wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ukawa na yule wa chama cha
mapinduzi CCM lakini hakuna anayefahamu vyema uwezo wa wagombea hao katika
kupambana na ufisadi hivyo ni vema wananchi wakawa makini katika kuchagua
kiongozi wao.
BOFYA HAPA KUSIKIA KAULI YA ZITTO KABWE.Akimzungumzia mgombea wa vyama vinayounda muungano wa ukawa Bwana. Zitto amesema mgombea huyo siyo msafi kama inavyoelezwa na viongozi wa vyama hivyo.
Makada wa
chama cha ACT waliohama kutoka chadema na kujiunga na chama hicho hivi karibuni
Chiku Abwao na Abuu Changawa walipata tabu kuhutubia mkutano huo baada ya
kukumbana na zomea zomea ya wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema waliokuwa
wakipinga hotuba zilizoonekana kuwashambulia viongozi wa chama chao.
0 comments:
Post a Comment