WATANZANIA saba wameula baada ya kuteuliwa kwenye kamati mbalimbali
za Shirikisho la Soka Afrika, (CAF). Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa
Shirikisho la Soka Tanznia (TFF), uteuzi huo ulifanyika kwenye kikao cha
Kamati ya Utendaji ya CAF kilichokutana mwishoni mwa wiki iliyopita
jijini Cairo, Misri.
Uteuzi huo utadumu kwa miaka miwili 2015-2017. Walioteuliwa ni Rais
wa zamani wa TFF Leodegar Tenga aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya
Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa
ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa
Kamati ya Ushauri na Vyama Wanachama.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameteuliwa kuwa Mjumbe Kamati ya
Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20, huku Katibu Mkuu
wa TFF akiteuliwa kuwa Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana
Umri chini ya miaka 17.
Mwingine ni Richard Sinamtwa aliyeteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya
Rufaa, Dk Paul Marealle -Mjumbe Kamati ya Tiba. Pia Mwenyekiti wa zamani
wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Lina Kessy ameteuliwa
kuwa Mjumbe ya Soka la Wanawake.
Kwa sasa Kessy ni Ofisa Michezo wa Umoja wa Afrika. Crescentius
Magori aliteuliwa kuwa Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la
Ndani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment