Mwanasiasa
huyo mkongwe nchini ambaye aliwahi kushika nyadhifa kadhaa katika
Serikali ya Awamu ya Kwanza, alifariki Dunia jana saa moja usiku katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mtoto wa marehemu,
Michael Kisumo alilithibitishia gazeti hili jana juu ya kifo cha baba
yake akisema kilitokana na maradhi ya figo ambayo yamekuwa yakimsumbua
kwa muda mrefu.
“Tulikuja hapa Muhimbili kwa ajili ya
mzee kufanyiwa dialysis (usafishaji damu katika figo) sasa ikajitokeza
complication (utata) akaanza kuharisha damu,” alisema.
Michael alisema baba yake alilazwa wodi ya kawaida juzi ili jana apatiwe tiba hiyo kabla ya hali yake kubadilika ghafla.
“Daktari
wake alipokuja leo (jana) na kumwangalia aliagiza atolewe wodi ya
kawaida ahamishiwe ICU lakini ilipofika saa moja usiku akatutoka”
alisema Michael.
Kifo cha mwanasiasa huyo kimekuja
takribani mwezi mmoja tangu arejee kutoka India ambako amekuwa akienda
mara kwa mara kuchunguzwa afya yake.
Hali ya ugonjwa
wake huo ilifikia katika kiwango cha juu na kulazimika kufanyiwa
uchujaji wa figo mara tatu kwa wiki kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.
Kisumo
aliwahi kuwa mmoja wa mameneja wa kampeni wa Rais Jakaya Kikwete mwaka
2005 akisimamia kanda ya kaskazini iliyojumuisha mikoa ya Kilimanjaro,
Arusha na Tanga.
Mbali ya kuwa waziri, aliwahi pia kuwa mkuu wa mkoa na mdhamini wa CCM.BOFYAHAPA->>http://bit.ly/1N6FCEr
0 comments:
Post a Comment