Kampuni ya Vodacom Tanzania
ambayo imekuwa ikidhamini ligi kuu ya Vodacom kwa miaka nane sasa imesaini
mkataba mwingine na TFF kuendelea kuidhamini ligi hiyo inayotarajia kuanza
kurindima Septemba 12 katika viwanja mbalimbali hapa nchini ambapo kila timu
itakuwa ikipata shilingi milioni 20 kila baada ya miezi mitatu.
Mkuu wa mawasiliano na masoko wa
Vodacom Tanzania Kelvin Twisha ameyataja maeneo yaliyofanyiwa maboresho kuwa ni
waamuzi na makamishna wa mechi ambao wameongezewa maslahi yao kwa asilimia 40
na kudai kuwa kampuni yake inajivunia kuwa wadhamini wakuu wa ligi hiyo maarufu
ndani na nje ya nchi inayofuatiliwa na mashabiki wa soka.
Naye afisa mtendaji mkuu wa bodi
ya ligi Boniface Wambura na rais wa TFF Jamal Malinzi wameahidi kufanya kila
liwezekanalo ili kuwa na ligi yenye ushindani zaidi pamoja na kuviasa vilabu
kujiepusha na migogoro na rushwa lakini pia wadau wengine wamehimizwa
kujitokeza kuongeza udhamini kwa vilabu au TFF ili kukidhi mahitaji ya vilabu
na uendeshaji wa ligi.
0 comments:
Post a Comment