Mmoja kati ya waratibu wa ukawa
Dr.George Kahangwa amesema katika makubaliano hayo majimbo 265 wamekubaliana
rasmi kuachiana na wagombea wengine ambao walipitishwa na tume ya taifa ya
uchaguzi lakini sasa wameenguliwa na vyama vyao wametakiwa kuheshimu uamuzi huo.
Naye mmoja kati ya wenyeviti wenza wa ukawa Bw.James
Mbatia ametetea kauli za mgombea wa
urais kupitia umoja huo kuhusiana na tamko lake kuhusu Masheikh wa Zanzibar
ambao wanakabiliwa na kesi pamoja mwanamuziki nguza vicking aliye kifungoni
kuwa lilikuwa linaashilia wataweka utawala wa sheria utakaochunguza pia uhalali
wa yaliyowasibu watu hao.
0 comments:
Post a Comment