Mgombea Mwenza waa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda alipowasili kwenye jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo, kuzungumza na kina mama wa makundi mbalimbali.
Mama Samia akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa wakati akienda ukumbini Kulia ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Albaert Mgumba.
Mama Samia akibishwa shuka nyeupe kuonyesha kukaribishwa kwa ukarimu na Kina mama wa Dodoma, kabla ya kuingia ukubini.
Mama Samia akibishwa shuka nyeupe kuonyesha kukaribishwa kwa ukarimu na Kina mama wa Dodoma, kabla ya kuingia ukubini.
Kinamama wakikoleza na kitenge kwenye shuka hiyo kumfanya Mama Samia ameremete zaidi kwa zawadi hiyo, kabla ya kuingia ukumbini.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akiwa katika picha ya pamoja na Kinamama waliompokea kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa (wanne kulia), kabla ya kuingia ukumbini.
Waalikwa wote wakiwa wamesimama ukumbini wakati Mama Samia akiingia
Shangwe zikitawala ukumbini wakati Mama Samia akiwasili ukumbini
Mama Samia akiwa tayari ukumbini.
Mama Samia akiwa na safu ya viongozi wengine meza kuu baada ya kuwasili ukumbini.
Mama Samia akiwasalimia waalikwa kabla ya kuketi.
Shamrashamra zikiendelea ukumbini.
Waalikwa wakiwa wametulia ukumbini kuanza shughuli.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma, Salome Kiwaya akimkaribisha Mama samia.
Mwakilishi wa kundi la wenye ulemavu akizungumza machache.
Mchumi wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Dodoma, Mwanahija Abdallah akizungumza kuhusu waliovyojiandaa kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Mmoja wa wajumbe waliopo katika kampeni za CCM, Ummy Mwalimu akieleza wasifu wa Mama Samia, akisema kuwa mbali ya kwamba ni mwanamke lakini Mgombea Mwenza huyo anazo sifa za ziada ambazo ni pamoja na kuwa Mwadilifu, Mchapakazi na mtu makini.
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Nkenge Kagera lakini akaanguka katika kura za maoni, Asupta Mshama akizungumza kuwaasa kinamama kutosusa chama wanapokosa kuchaguliwa badala yake waiunge mkono CCM iendelee kushinda uchaguzi
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma, Fatuma Mwenda akimzawadia Mama Samia kitenge.
Kisha aakamkumbatia kwa furaha.
Mama Tunu Pinda akizungumza mambo mbalimbali ikiwemo kuwahakikishia wenzake kwamba Mumewe Waziri Mkuu Mizengo Pinda hawezi kuhama CCM katu, na kwamba ikitokea akamaha yeye ataachana naye ili abaki CCM. Pia amewahimiza kina mama kuhakikisha wale wote waliohama CCM kwenda upinzani wanakatwa hukohuko waliko wakati wa Uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Adam Kimbisa akizungumza ukumbini.
Mama Samia akiwahutubia Kina mama katika mkutano huo.
Mama Samia akiwahutubia kina mama katika mkutano huo.
Kina Mama wakimsikiliza kwa makini Mama Samia alipokuwa akiwahutubia
Kina mama wakimsikiliza kwa makini na utulivu mkubwa Mama Samia Suluhu Hassani alipokuwa akizungumza nao katika ukumbi uliopo jengo la White House Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma leo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment