Mkoa wa Shinyanga
umebainika una idadi kubwa ya watoto wenye udumavu wa afya na utapiamlo hali
inayosababishwa na ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi kwa wananchi wa mkoa huo
na Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa asilimia thelathini ya watoto wote
wenye umri chini ya miaka mitano wamedumaa.
Hayo yamesemwa na katibu tawala wa
wilaya ya kishapu Bw.Shadrack Kengese kwa niaba ya mkuu wa mkoa washinyanga
katika maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyofanyika kimkoa katika
kata ya ukenyenge wilaya ya Kishapu huku akiwataka wanawake kujenga tabia ya
kunyonyesha watoto wao hadi kufikia umri wa miaka miwili na kuendelea ili
kujenga familia yenye nguvu na isiyosumbuuliwa na maradhi.
Afisa mahusiano wa shirika la SAVE
THE CHILDREN mkoa wa Shinyanga Bw. Petro Mahui amesema lengo la maadhimisho
hayo ni kuhakikisha jamii nzima inaweka mikakati ya kushiriki kikamilifu katika
kupiga vita utapiamlo na udumavu wa afya kwa watoto chini ya umri wa miaka
mitano hali itakayoliwezesha taifa kukua kiuchumi na kufikia malengo ya
milenia.
Kwa upande wake afisa mwezeshaji
taasisi ya chakula na lishe mkoa wa shinyanga Bi.Debora Charwe amewataka wadau
wa afya nchini kuhakikisha elimu ya unyonyeshaji kwa kipindi kinachoshauriwa
inawafikia walengwa wote huku akiwataka waajiri kutoa nafasi maalum kwa
waajiriwa wanawake wanaonyonyesha kuendelea kufanya hivyo mahala pa kazi kama
sheria inavyoelekeza.
0 comments:
Post a Comment