Vikosi vya usalama vya Sudan
Kusini vimepiga marufuku kituo kimoja cha redio na mashirika
mawili ya magazeti kuendesha shughuli zao za kazi.
Miongoni mwa mashirika hayo ya
habari yaliyowekewa marufuku ni gazeti la Al-Rai la lugha ya
Kiarabu, The Citizen la Kiingereza pamoja na kituo cha redio cha
sauti ya uhuru kinachorusha matangazo katika mji mkuu wa Juba nchini Sudan
Kusini.
Ingawa vikosi vya usalama vimezuia
mashirika hayo kuendesha shughuli zao, serikali ya Sudan Kusini bado
haijatoa maelezo rasmi kuhusiana na ilani ya marufuku.
Kwa upande mwingine, mashirika
hayo yanadaiwa kupigwa marufuku kutokana na sababu za kiusalama nchini
humo.
Kamati ya Umoja wa Ulaya iliyoko Sudan
Kusini imeripotiwa kutoa tahadhari kwa serikali ya nchi kutokana na suala
hilo.
0 comments:
Post a Comment