Shirika la Umoja wa Mataifa lilichukua uamuzi wa kuunda jopo jipya la kuchunguza wahusika wanaotengeneza silaha za kemikali nchini Syria.
Jopo hilo linatarajiwa kuwa na wanachama 15.
Syria ni nchi ambayo imekuwa ikikumbwa na vita kwa muda wa miaka 5 na kusababisha kufariki kwa wananchi wasiopungua 250,000.
Wanachama walilisisitiza kuwa jopo hilo litafanya uchunguzi ya vyombo ambavyo vinatumika kutengeza kemikali, wahalifu serikalini na wadhamini wa silaha hizo.
İmebainika kwamba kemikali aina ya klorini hutumiwa nchini Syria.
0 comments:
Post a Comment