Image
Image

Serikali ya Sierra Leone kufutilia mbali baadhi ya vikwazo vilivyowekewa wananchi kutokana na janga la Ebola.


Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma, ametangaza kwamba serikali imechukua uamuzi wa kufutilia mbali baadhi ya vikwazo vilivyokuwa vimewekewa wananchi kutokana na janga la Ebola.
Akizungumza kwenye kituo cha redio na televisheni, Koroma alifahamisha kuchukuliwa kwa uamuzi huo kufutilia hali ya utulivu iliyorudi nchini humo.
Baadhi ya vikwazo vilivyowekwa hapo awali vilikuwa ni marufuku ya mikutano ya hadhara, michezo, mikahawa ya burudani za usiku na mengineyo.
Vikwazo vya kibiashara kama vile usafiri wa pikipiki na masoko ya umma pia vitaondolewa ingawa vikwazo hivyo vitazingatiwa siku za Jumapili.
Koroma aliongezea kusema kwamba Ebola ni ugonjwa sugu usioweza kutabirika, huku akitoa tahadhari kwa wananchi kuwa waangalifu zaidi ili kuepukana na kuzuka kwa kesi mpya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment