Polisi wa Uhispania wametekeleza operesheni na kuwatia mbaroni washukiwa 36 wa ulanguzi wa madawa ya kulevya katika visiwa vya Canary.
Polisi hao pia wanaarifiwa kukamata kilo 342 za madawa ya kulevya katika operesheni hiyo iliyotekelezwa siku ya Ijumaa.
Wakati huo huo, takriban fedha dola milioni 1.1 pia zilipatikana baada ya ukaguzi kufanyika katika vituo saba vya maficho.
Washukiwa hao wanasemekana kuingiza madawa ya kulevya kutoka Colombia, na kuyaficha ndani ya shehena ya mizigo halali kabla ya kupanga kuisafirisha nchini Brazil kupitia visiwa vya Canary.
0 comments:
Post a Comment