Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mashahidi wa
tukio hilo waliripoti kuwa eneo moja ililipuliwa na kusababisha shimo lenye
kina kirefu cha mita 10.
Majumba kadhaa yaliharibika kutokana na mlipuko
huo.
Waziri wa afya wa Afghanistan alifahamisha kuwa
taarifa hiyo ilitolewa na hospitali ambazo ziliwapokea majeruhi kwa ajili ya
matibabu.
Waziri huyo alifahamisha kuwa zaidi ya watu 400 ndio
waliojeruhiwa.
Maafisa wa serikali walisema kuwa wanaendelea
kufanya uchunguzi wa chanzo na watekelezaji wa mlipuko huo.
İnasemekana kwamba bomu hilo lilikuwa na nguvu
isiyokuwa ya kawaida kwenye eneo ambalo hulengwa na kundi la Taliban na
wanamgambo waliokuwa na lengo la kudhoofisha serikali ya Afghanistan.
0 comments:
Post a Comment