Babake mtoto wa kipalestina aliyechomwa moto hadi kufariki wiki iloipita afariki.
Sa'ad Dawabsheh babake mtoto wakipalestina aliechomwa mot ona walowezi wa kiyahudi katika ukingo wa magharibi amefariki katika hospitali ya Soroka Israel.
Dawabsheh alipelekwa hospitali baada ya kuungua katika shambulizi la moto lilisababisha mtoto wake kufariki kwa kuchomwa moto.
Mke Dawabsheh, bi Riham na mwana wao Ahmad bado wako katika hali mahututi hospitalini baada ya nyumba yao kuchomwa moto.
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu aliahidi kuwa waliohusika na shambulio hilo kukamatwa na kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria.
0 comments:
Post a Comment