Image
Image

Rais Buhari atoa agizo la uundaji wa silaha kwa Wizara ya Ulinzi nchini Nigeria.


Rais wa Nigeria Muhammed Buhari, ametoa agizo la kuanzishwa kwa shughuli ya uundaji wa silaha kwa Wizara ya Ulinzi nchini ili kusaidia mapambano dhidi ya kundi la Boko Haram.
Akitoa hotuba yake kwenye hafla ya chuo cha kijeshi iliyoandaliwa katika mji mkuu wa Abuja, Buhari alisema, ‘‘Hatuwezi kuruhusu vifaa vya jeshi la Nigeria kuletwa kutoka nje.’’
Buhari alitoa agizo hilo huku akibainisha kwamba Wizara ya Ulinzi ya Nigeria itaanza kufanya maandalizi kwa ajili ya uundaji wa silaha za ndani.
Nchi nyingi za kimataifa zikiwemo Marekani na Uingereza, zilisitisha mauzo ya silaha kwa Nigeria kwa kuhofia matumizi mabaya na ukiukaji wa haki za kibinadamu nchini humo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment