WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imehimiza vijana
kuhakikisha wanachagua viongozi wenye maslahi kwa taifa katika uchaguzi
mkuu Oktoba 25, mwaka huu. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa
Elisante Ole Gabriel alitoa mwito huo jijini Dar es Salaam jana katika
maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani.
Aliwataka vijana watumie haki yao ya msingi, kupiga kura na kuchagua
wanaowahitaji na ambao wataleta maendeleo nchini. “Chagueni viongozi
wenye maslahi kwa taifa kwani kura zenu ndio zenye kuonesha mnahitaji
Tanzania ya aina gani,” alisema Profesa Gabriel.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA), Dk. Natalia
Kanem alisema kwa Tanzania wapo vijana milioni 1.8 kwa mujibu wa Sensa
ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
Aliwataka vijana kutumia wingi wao kuwa imara na kuwa sehemu ya
uamuzi, kushiriki katika ngazi za maendeleo, kutambua ndoto zao na
kuzitumia ipasavyo katika kukuza uchumi.
“Ushiriki wa vijana ni suala la haki za binadamu… asilimia 90 ya
vijana wanaishi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hivyo waamke
na kuwa chachu ya maendeleo,” alisema Dk. Kenan. Akisoma mapendekezo ya
vijana, Hussein Melele alisema ni wakati sasa kwa serikali kuhakikisha
inawashirikisha kwenye nyanja mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment