Agosti 5 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitia saini sheria tano
zilizopitishwa na Bunge hivi karibuni licha ya kupingwa na wabunge wa
upinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Rais Kikwete alitia saini Sheria ya Mafuta na Gesi; Sheria ya Uwazi
na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini; Mafuta na Gesi Asilia
Tanzania; Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi; Sheria ya
Tume ya Walimu na Sheria ya Masoko ya Bidhaa zote za mwaka 2015.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (pichani),
aliyaeleza hayo jana wakati wa mkutano na wadau mbalimbali na wakuu wa
mashirika ya mafuta na gesi, wakati wakijadili sheria hizo na jinsi
zinavyoweza kuwanufaisha Watanzania.
“Serikali inatambua tuko kwenye zama za gesi ambayo ni rasilimali
kubwa, yenye thamani haina maana kama hatutawaeleza Watanzania namna ya
watakavyonufaina na rasilimali hiyo kubwa, pia tunatambua mchango wa
mashirika binafsi katika sekta hii na pia sheria hizi zimekuwa za uwazi,
” alisema Mwijage.
0 comments:
Post a Comment