SHIRIKISHO la Mpira la Soka Tanzania (TFF) limesaini mkataba mpya wa
miaka mitatu wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao na kampuni
ya simu za mkononi ya Vodacom.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amethibitisha kusainiwa kwa
mkataba huo na kusema hawakufanya sherehe za kutia saini mkataba huo
kutokana na mashindano ya Kagame yaliyokuwa yanaendelea nchini kwani TFF
ndio iliyokuwa ikiyasimamia kama shirikisho la soka mwenyeji.
“Wanasema katika ajira, unaposikia nafasi haijatangazwa na
hajatangazwa mtu mpya basi kuna maendeleo na mara nyingi mkataba
unaoendelea uliokuwepo ukisainiwa tena ‘renewal contract’ haivuti
masikioni kama unapoongelea mkataba ambao watu wameingia udhamini mpya,”
alisema Mwesigwa.
Pia Mwesigwa aliweka wazi kuwa mdhamini wa ligi msimu unaokuja ni
Vodacom ambao walikuwepo msimu uliopita kwani kila kitu kimeshawekwa
sawa ila kwa maana ya sherehe ndio bado haijafanyika kwasababu kulikuwa
na mambo mengi hapa katikati ikiwa ni pamoja na mashindano ya Kagame.
Pamoja na kukiri kuwa TFF imeshakubaliana na Vodacom kuendelea kwa
miaka mitatu ijayo, lakini hakuweka wazi jinsi mkataba huo
ulivyoboreshwa kwa madai hadi sherehe za kutiana saini zitakapofanyika.
“Mkataba ni miaka mitatu, kutakuwa na ongezeko ukizingatia kuna timu
zimeongezeka lakini nadhani hata kile kinachokwenda kwenye klabu
kitaongezeka kwa kiasi fulani, lakini siwezi kuzungumza kwa undani kwa
sasa.
Pia kwa upande wa kwetu tulikuwa na mambo ambayo tuliyaona hayapo
sawa, hivyo kulikuwa na muda mwingi wa kutosha kujadili karibu miezi
nane iliyopita kwa hiyo vitu vingi vimeangaliwa,” alisema Mwesigwa.
Vodacom wamekuwa wakidhamini ligi kuu lakini kumekuwepo malalamiko
mengi kwa klabu kuwa kiasi wanachotoa hakitoshelezi ukizingatia baadhi
ya timu hazina mfadhili
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment