PILIKAPILIKA za usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL), zinafikia tamati
leo saa 6:00 usiku, imeelezwa. Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Baraka Kizuguto alisema kuwa TFF imezikumbusha klabu zote
zinazoshiriki msimu mpya wa mwaka 2015/2016, kuhakikisha vinakamilisha
usajili wa wachezaji wao kabla ya dirisha hilo la usajili kufungwa.
Kipindi cha dirisha la usajili kwa timu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza
na Ligi Daraja la Pili kilifunguliwa Juni 15, 2015 na kitamalizika leo
kwa awamu ya kwanza. Timu hasa zile zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara
zimekuwa katika heka heka kubwa ya usajili kuhakikisha zinaimarisha
zaidi vikosi vyao ili viweze kufanya vizuri katika msimu ujao.
Mbali na kusajili wachezaji wa ndani baadhi ya klabu kama Simba,
Yanga na Azam FC wamejiingiza pia katika usajili wa wachezaji kutoka nje
ili kuviongezea nguvu vikosi vyao.
TFF imeruhusu wachezaji saba kusajiliwa na klabu za Tanzania na
kuweza kuwatumia wote kwa wakati mmoja katika mchezo baada ya msimu
uliopita kuruhusu timu kusajili wachezaji watano. Hata hivyo,awali timu
ziliomba kuruhusiwa kusajili hadi wachezaji 10 wa kigeni, lakini TFF
ikaruhusu wachezaji saba tu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment