Wagombea ubunge wa Jimbo la Mtwara Mjini wameaswa kufanya kampeni za ustarabu wakati utakapowadia ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu na miongozo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi lengo likiwa kuondokana na vurugu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Mtwara Mjini, Bwana AMBAKISYE SHIMWELA baada ya kutoa fomu kwa wagombea ubunge kutoka Chama cha Wananchi - CUF na NCCR- Mageuzi.
Amesema wasimamizi wa uchaguzi wanahitaji kuona wagombea wa vyama vyote wanafanya kampeni za ustarabu ikiwa ni pamoja na kufuata kanuni na miongozo ambayo ameitoa kwa kila mgombea.
Amesema ofisi yake inawajibu wa kumkabidhi kila mgombea vitendea kazi ikiwa ni pamoja na fomu namba kumi ambayo inamtaka mgombea kukiri atafuata maadili yaliyoainishwa kwenye kitabu cha maadili ya uchaguzi ya mwaka 2015.
Bwana SHIMWELa amesema mpaka sasa jimbo la Mtwara Mjini ni wagombea wawili ndiyo wamejitokeza kuchukua fomu za ubunge ambao mwisho wa kuchukua na kurejesha ni tarehe 21 ya mwezi huu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment