Mkutano mkuu wa wakulima wa korosho wakiwemo wadau wa zao hilo umemalizika wakiwa wamekubaliana kwa sauti moja bei mwongozo kwa msimu wa mwaka huu 2015-2016 ni Shilingi Elfu-Moja na 200.
Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Bodi ya kurosho nchini, ANNA ABDALLAH amesema bei hiyo siyo ya soko bali korosho ipande ama ishuke mkulima atalipwa kiasi hicho cha pesa kwa kila kilo moja ya korosho.
Amebainisha kuwa msimu wa mwaka jana 2014-2015, bei mwongozo ilikuwa Shilingi Elfu-Moja, lakini bei ya soko kwa kilo moja iliuzwa Shilingi Elfu Moja na 400hadi miatano bei ambayo amesema ilikuwa nzuri.
Amesema ana imani mwaka huu bei itakuwa nzuri hivyo amewaasa wakulima kuuza mazao yao kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani badala ya kukopa kwenye mabenki ambayo yamewarudisha nyuma katika maendeleo.
Mkutano huo pia umetumika kuchagua bodi mpya ya wadhamini ambayo hushughulika na kukusanya michango ya wadau ambayo hutumika kugharamia shughuli za pamoja, na inafahamika kwa jina la mfuko wa kuendeleza zao la korosho nchini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment