Image
Image

Van Gaal Bado anaimani na Sergio Romero


Meneja wa Klabu Ya Manchester United Louis Van Gaal amemtete mlinda mlango wake Sergio Romero kutokana na lawama anazotupiwa mlinda mlango huyo kwa kusababisha kipigo cha mabao 2 kwa 1 kwenye ligi kuu yay a Uingereza dhidi ya Swansea mchezo uliopigwa jana jumapili.

Dadika tisini zilipoisha zilisika kelele za mashabiki kutaja jina la David De Gea aliyekuwa mlinda mlango namba moja wa Manchester united msimu uliopita ikiwa ishara ya kumtaka mlinda mlango huyo apewe nafasi tena, lakini Van Gaal alisema haoni sababu ya kumchezesha De Gea wakati Sergio Romero ana uwezo mkubwa na kilichotokea jana ni uzembe wa safu nzima ya ulinzi.

Juan Mata alinza kuifungia Manchester United goli kabla ya Andre Ayew kuisawazishia Swansea huku naye Bafetimbi Gomis’ akipachika goli la pili na la ushindi.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment