Watu 24 wamekufa na wengine 25
wamejeruhiwa huko India baada ya treni mbili za mwendo wa kasi kuacha njia na
kutumbukia kwa kufuatana kwenye mto uliokuwa umefurika.
Treni hizo zilizohusika na ajali
katika Jimbo la Madhya Pradesh zilikuwa zinavuka daraja la moto uliokuwa
umerika na makundi ya uokoaji yanasema mvua inayoendelea ilikuwa inakwamisha
shughuli za uokoaji.
Taarifa zinasema katika hiyo
iliyotokea kilomita 950 kutoka mji mkuu wa India, Delhi mabehewa yametumbukia
katika mto na watu 300 waliokuwa kwenye treni hizo wameokolewa.
Msemaji wa reli ameeleza kuwa
treni iliyokuwa inatoka Varansi kwenda Mumbai ilikuwa yakwanza kutumbukia
kwenye mto na kufuatiwa na iliyokuwa inatoka upande mwingine iliyoanguka muda
mfupi baadaye.
0 comments:
Post a Comment