9 wauawa, wengi watekwa nyara na washambuliaji wanaoaminika kuwa wanamgambo wa Boko Haram.
Watu 9 wameripotiwa kuuawa na wengine wengi wakiwemo watoto kuchukuliwa mateka katika kijiji kimoja kilichokuwa mpakani mwa Cameroon na Nigeria.
Viongozi wa Cameroon wamelihusisha kundi la Boko Haram na mashambulizi hayo.
Washambuliaji hao wanasemekana kutekeleza mashambulizi hayo kwa kutumia malori ya kutoka Nigeria.
Uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaarifiwa kuanzishwa na maafisa wakuu.
Hapo awali, kundi la Boko Haram liliwahi kutangaza kwamba linapanga kufanya mashambulizi nchini Cameroon.
0 comments:
Post a Comment