TIMU ya Yanga ya Dar es Salaam imezidi kuzitambia timu za Mkoa wa
Mbeya, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, katika mechi ya
kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Yanga ambayo michezo ya awali ilizifunga Kimondo kutoka Mbozi kwa
mabao 4-1, kisha Tanzania Prisoni mabao 2-0, wakati jana iliibamiza
Mbeya City mabao 3-2.
Katika mchezo huo, Mbeya City ilikuwa ya kwanza kujipatia bao
lililofungwa na Bakari Mwijuma, baada ya kumzidi akili mlinda mlango wa
Yanga, Ally Mustapha na kuzitikisa nyavu dakika ya nane.
Yanga ambayo ilijaza viungo wengi, ilijibu mashambulizi
yaliyoiwezesha kusawazisha bao hilo lililofungwa na Andrey Coutinho,
dakika ya 17.
Amis Tambwe aliwainua mashabiki wa Yanga kwa kuandika bao la pili
dakika ya 45, akitumia vizuri mpira wa krosi uliopigwa na Donald Ngomana
kuunganisha kwa kichwa na kuwa bao.
Yanga ilikianza kipindi cha pili kwa kulisakama lango la wapinzani
wao, dakika ya 49, Mzimbabwe Donald Ngoma aliwainua mashabiki wao kwa
kufunga bao la tatu baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Mbeya
City.
Mchezaji aliyetokea benchi, Meshaki Abel, aliiandikia timu ya Mbeya
City bao la pili dakika ya 90, baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Yanga
na kuachia shuti kali lililomshinda kudaka kipa wa Yanga, Mustapha.
Yanga iliwatoa Vicent Bisou, Thaban Kamuoko, Simon Msuva, Amis
Tambwe, Donald Ngoma na Andrey Coutinho na kuwaingiza Mbuyu Twite, Deus
Kaseke, Malimi Bisungu, Said Juma, Godfrey Mwashiuya na Mateo Antony.
Kwa upande wa Mbeya City, iliwatoa John Kabanda, Hassan Mwasapili,
Steven Mazanda, Hassan Seleman, Bakari Mwijuma na Joseph Mahundi na
kuwaingiza Salvatory Nkulula, David Lukoku, Hamad Omary, Richard Peter,
Meshack Samwel, Geophrey Mlawa na Hamad Kibopile.
0 comments:
Post a Comment