Watu 15 wameuawa na wengine 30 wamejeruhiwa huko Brazil baada ya basi kuanguka karibu na mji wa enzi ya ukoloni wa Paraty.
Maafisa wamesema basi hilo lilianguka kwenye kona kali ya mteremko na baadhi ya majeruhi walichukuliwa kwa helikopta kuwapeleka kutibiwa hospitali za karibu.
Inasemekana mahali ilipotokea ajali hiyo kwenye mteremko wa mlima ni pabaya na hatari
sana na panaitwa na wenyeji kama mahali pa kuomba MUNGU NISAIDIE.
Na huko Afrika ya Kusini watu 15 wamejeruhiwa wakati basi dogo lilipoanguka barabara
moja kando ya mji wa Johannesburg baada ya dereva wake kushinda kulidhibiti.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment