SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) lipo katika mchakato wa kumpa Mkataba wa kudumu,
kocha wa muda wa timu ya taifa, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa.
Pamoja
na kucheza mechi tatu bila kushinda, lakini TFF imeridhishwa na
maendeleo ya timu kutoka ilivyokuwa chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij
na imeshawishika kumpa Mkataba wa kudumu Mkwasa.
Kiwango
kizuri ambacho timu ilionyesha katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya
Nigeria kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ndicho
kimeifanya TFF ifikirie hilo.
Aidha,
TFF pia baada ya kukusanya maoni ya wachezaji mmoja na wote kuridhishwa
na benchi la Ufundi la sasa la timu- inaona hakuna sababu ya kutowapa
Mkataba wa kudumu Mkwasa na benchi lake.
Washambuliaji
wawili wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta pamoja
na Nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga SC ya nyumbani walisema
timu imebadilika chini ya Mkwasa.
Viungo Himid Mao wa Azam FC na Said Ndemla wa Simba SC nao walisema timu imebadilika mno kutoka ilivyokuwa chini ya Nooij.
Lakini
inafahamika Mkwasa ni kocha wa Yanga SC anayefanya kazi na Mholanzi,
Hans van der Pluijm na kuhusu hilo, klabu hiyo imesema haina shida
kumuachia.
Katibu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha amesema kwamba wako tayari kumuachia Mkwasa akafanye majukumu ya kitaifa.
“Tunachoomba
tu TFF wafuate utaratibu wa kuvunja mkataba, ana Mkataba na sisi wa
miaka miwili, ambao ameutumikia kwa miezi minane tu,”amesema Tiboroha.
Rais
wa TFF, Jamal Malinzi alimteua Mkwasa kukaimu Ukocha Mkuu Taifa Stars
kwa miezi mitatu tangu Julai na akasema kwa kuanzia atakuwa anachukua
mshahara alikuwa analipwa Nooij.
Nooij
aliyekuwa analipwa dola za Kimarekani 12,500 (zaidi ya Sh. Milioni 25)
kwa mwezi, alifukuzwa mwishoni mwa Juni baada ya Taifa Stars kufungwa
mabao 3-0 na Uganda Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mechi ya kufuzu
CHAN.
“Kocha
Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho)
alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua
benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa
mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao
wazawa” alisema Malinzi wakati anamtangaza Mkwasa.
Mkwasa
aliwateua Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ kuwa Mshauri wa
Ufundi, Hemed Morocco kuwa Kocha Msaidizi na Manyika Peter kuwa kocha wa
makipa wakichukua nafasi za Salum Mayanga na Patrick Mwangata.
Aidha,
Omar Kapilima aliteuliwa kuwa Meneja na Hussein Swedi ‘Gaga’ kuwa
mtunza vifaa vya timu- kukamilisha sura mpya kabisa ya benchi la Ufundi
la Taifa Stars.
Na
tangu hapo timu imcheza mechi tatu bila ushindi ikitoa sare ya 1-1 na
Uganda mjini Kampala kufuzu CHAN, ikifungwa 2-1 na Libya mchezo wa
kirafiki mjini Kartepe, Uturuki na kutoa sare ya 0-0 na Nigeria mwishoni
mwa wiki.
Hayo
yalikuwa mabadiliko makubwa kutoka kwenye timu kufungwa mechi tano
mfululizo na kwa ujumla kucheza mechi 11 bila ushindi chini ya Nooij.
Crdt:Mahmoud Zubeiry
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment