Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo, ANNA MGHWIRA amesema, chama hicho katika ilani yake kimetoa kipaumbele katika kilimo ili kuhakikisha wakulima nchini wanawezeshwa kulima kisasa, kusindika mazao na kuuza ili kuwakomboa wananchi zaidi ya asilimia 80 ambao wanategemea kilimo.
Akihutubia katika mkutano wa kampeni akiomba kura za kuchaguliwa kuwa Rais, katika Mji wa Namanyere Wilayani Nkansi Mkoani Rukwa, ANNA MGHWIRA amesema chama hicho kimefanya tathmini na kuweka vipaumbele katika sekta ya kilimo ambavyo ni kuhahakikisha mkulima hakopwi mazao, pembejeo zinapatikana na kuwepo kwa fao la bei ya mazao.
Akizungumzia uadilifu katika mkutano wa kampeni mjini Sumbawanga, amesema chama hicho kitarudisha misingi ya uadilifu ili kuleta maendeleo.
Kwa upande wake mgombea ubunge wa ACT Wazalendo Sumbawanga Mjini, EMMANUEL MSENGEZI amesema msimamo na sera ya act katika kusimamia utu, uzalendo na uadilifu unakifanya chama hicho kiwe tofauti na vyama vingine.
Home
News
ACT- Kutoa kipaumbele katika kilimo ili kuhakikisha wakulima nchini wanawezeshwa kulima kisasa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment