Image
Image

Wakazi wa majimbo ya Isimani na Kalenga kurejeshewa mashamba yao yaliyobinafsishwa kwa wawekezaji - CHADEMA.

Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA , JUMA DUNI  HAJJI, amewaahaidi wakazi wa majimbo ya Isimani na Kalenga kwamba wakiingia madarakani watarejeshewa mashamba yao  yaliyobinafsishwa kwa wawekezaji na wamesshindwa kuyaendeleza.
Katika mikutano ya kampeni mgombea mwenza huyo  ameendelea kunadi sera za chama hicho na kumuombea kura mgombea wake wa Urais EDWARD LOWASSA kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa.
Akihutubia mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu katika majimbo ya Isimani na Kalenga JUMA DUNI  HAJJI amesema iwapo Watanzania watamchagua LOWASSA, atahakikisha wakulima na wafugaji wanaingizwa katika mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kukomesha migogoro pamoja na kuwajengea mazingira mazuri wafanyabiashara ndogondogo kwa kuwaondolea utitiri wa kodi ambazo zinadaiwa kuwanufaisha baadhi ya watu wachache.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani kupitia CHADEMA PATRICK ole SOSOPI  amesema akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha maisha ya wananchi wanaoishi jirani na Hifadhi ya taifa ya Ruaha yanakuwa ya amani na furaha.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment