Image
Image

Ahmed Mohamed apokea mwaliko wa rais Obama.


Kijana aliyekamatwa na polisi kwa ajili ya kuleta saa aliyoitengeneza iliyodhaniwa kuwa bomu aachiliwa na kupata mwaliko rasmi kutoka kwa rais Obama katika Ikulu ya Marekani
Ahmed Mohamed ni kijana wa umri wa miaka 14 anayeishi Texas alishutumiwa na maafisa wa polisi kutengeneza bomu.
Wakati huo huo, mkurugenzi wa Facebook Mark Zuckerberg pia alimwalika Ahmed kumtembelea katika kampuni yake iliyokuwa makao makuu yake Carlifonia.
Mark pia aliandika ujumbe kwenye Facebook ulisoma, ‘‘Umiliki wa kipaji cha ubunifu wa kuunda kifaa kizuri unapaswa kuleta sifa na wala sio kukamatwa.’’
Tukio la kukamatwa kwa Ahmed limezua gumzo kwenye mitandao ya jamii na kupelekea kuanzishwa kwa kampeni ya #IStandWithAhmed katika jukwaa la Twitter.
Baraza la mambo yanayohusiana na dini ya kiislamu Marekani lilishutumu vikali tukio hilo na kusema kuwa ni mfano tosha wa chuki kwa waislamu nchini.
Hata hivyo msemaji wa polisi James McLellan alikanusha madai ya baraza hilo na kusisitiza kwamba dini ya Ahmed haikuwa na uhusiano wowote na kitendo chao cha kumkamata kijana huyo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest alisema kuwa Ahmed amealikwa katika Ikulu hiyo ili aweze kushiriki katika elimu ya nyota pamoja na wanaanga wa NASA.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment