Jeshi la Marekani pamoja na wakazi wachache wa Diffa walifanya mkutano ya watu wasiopungua 20 ili kujadiliana kuhusu uendeshaji wa mapambano dhidi ya Boko haram kwa kutumia mkakati mpya wa rais Obama dhidi ya ugaidi
Licha ya miaka mingi ya vitisho na vurugu zinazosababishwa na mashambulizi ya mara kwa mara na wanamgambo wa Boko haram,wakazi wa maeneo ya Diffa nchini Niger hawajawahi kuunda mbinu maalum za kupambana na kundi hilo haramu.
Watu wengi wanahofia maisha yao kwani wanawaona wanamgambo hao kuwa hatari sana.
Mpango mpya wa kupambana na ugaidi hautahitaji silaha kwani jeshi la marekani linawasaidia vijana wa Diffa kuunda mbinu maalum za kuwazuia wanamgambo hao kuenea Niger na pia askari hao wanafanya operesheni zao wakiwa wamevalia nguo kama raia wengine wa kawaida.
Mbinu hiyo mpya ilitangazwa na rais wa Marekani Obama mnamo mwezi Mei mwaka 2014 dhidi ya makundi ya kigaidi.
Mbinu hiyo tayari imezaa matunda katika sehemu ingine nchini Niger.
0 comments:
Post a Comment