Albino kama huyu wamekuwa wakilengwa nchini Tanzania.
Watu wasiojulikana wanaripotiwa
kujaribu kukata sehemu za mwili za mwanamme mmoja mwenye ulemavu wa
ngozi au albino nchini kenya, kisa ambacho kimezua hali ya wasiwasi kuwa
huenda albino wakalengwa hasa kutoka nchini Tanzania.
Akiongea na
gazeti moja nchini Kenya, Enock Jamenya mwenye umri wa miaka 56,
alisema kuwa watu watatu walimvamia nyumbani kwake katika wilaya ya
vihiga magharibi mwa kenya, ambapo walimuitisha pesa.
Alipowambia hana pesa za kuwapa watu hao walimuomba sikio au mkono wake ili wapate kuuza nchini Tanzania.
Kulingana na gazeti hilo , watu hao walijaribu kumkata sikio ,mkono
na vidole na kisha wakakimbia na kumuacha Jamenya akiwa na majeraha
mabaya.
Katika nchi jirani ya Tanzania baadhi ya wanasiasa wamelaumiwa kwa kununua viungo vya albino ili kutumia kufanyia uchawi.
Makundi
ya kutetea haki za binadamu , yameonya kwa kuna hatari ya kuongezeka
kwa mashambulizi dhidi ya albino nchini Tanzania wakati huu wa kampeni
za uchaguzi mkuu.
Takrian albino 76 wameuawa nchini Tanzania tangu
mwaka 2000, huku sehemu zao za mwili zikiuzwa kwa dola 600 na mwili
mzima ukiuzwa na kwa dola 75,000 kwa mujibu wa wataalamu wa umoja wa
mataifa.
0 comments:
Post a Comment