Chama
cha mapinduzi (CCM) katika wilaya ya Bukoba mjini kimepata pigo baada ya baadhi
ya viongozi wa kata ya Kahororo na baadhi ya wanachama katika kata
hiyo kukihama katika chama hicho na kumfuata Chief Kalumuna aliyechukua uamzi wa kujiengua CCM na
kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) baada
ya jina lake kukatwa kimizengwe pamoja na kuibuka mshindi kwanza wa
kinyanganyiro cha kura za maoni.
Baadhi
ya viongozi waliokihama chama hicho katika kata hiyo ya Kahororo ni pamoja na
katibu ,Mweka hazina, mchumi, mwenyekiti na wajumbe wa sekretarieti
ya chama hicho,viongozi hao walitangaza adhima yao ya kuihama CCM wakati
wa mkutano wa kampeni uliondaliwa na chadema kwa kushirikiana na vyama
vinavyounda umoja wa ukawa ambao umefanyika kwenye viwanja vya mtaa wa Kyaya
uliko katika kata ya Kahororo, katika manispaa ya Bukoba.
Pamoja
na kuelezea sababu zilizowapelekea kujiengua CCM na kujiunga na Chadema
viongozi hao na baadhi ya wanachama waliojiengua walimkabidhi mgombea wa
udiwani kata ya Kahororo Chief Kalumuna kaliyekuwa pia mwenyekiti wa
vijana wa CCM wilaya ya Bukoba mjini kadi za uanachama zaidi ya mia
mbili na navitendea kazi mbalimbali walivyokuwa
wakivitumia kuinadi CCM ambavyo ni pamoja na bendera.
Katika
mkutano huo meya wa zamani wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani
amewaomba wananchi wawachague wagombea wanaowania nafasi za uongozi kwa lengo
la kutetea maslahi ya wananchi na ambao hawana taswira ya kukwamisha
maendeleo huku mgombea wa ubunge kupitia tiketi ya Chadema Wilfred Lwakatare akiwaeleza
wananchi kuwa akichaguliwa atakuwa mbunge wa kubuni mikakati ya kuwawezesha
wananchi kuondoka na hali ya utegemezi.
Mkutano
huo ulipambwa na burudani mbalimbali toka kwa wasanii, burudani hizo zilikuwa
zikiwakuna wagombea ambapo wakati mwingine walilazimika i kujimwaga
uwanjani kucheza sambamba na wananchi.
0 comments:
Post a Comment