Serkali Wilayani Arumeru imesema itawachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria pamoja na kuwafikisha mahakamali, wazazi wote watakao aozesha wanafunzi waliokamilisha elimu ya msingi hivi karibuni ili kukomesha tabia ya kuwadhulumu watoto haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, FIDELIS RUMATO alipokuwa akizungumza katika hafla ya kuwahamasisha wanafunzi kujikita katika masomo ya sayansi, kwa lengo la kupata wataalamu pamoja na waalimu wa masomo hayo.
Wakizungumza na Radio One Stereo baadhi ya wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi wameiomba jamii kuwa karibu na watoto wao kwa kipindi hiki cha kusubiri matokeo ili kuwaepusha na makundi mabaya ikiwamo kujihusisha na utumiaji wa dawa ya kulevya.
Kwa upande wao wadau wa elimu Wilayani Arumeru wameitaka serkali kuiboresha elimu ya Tanzania ili kuondokana na tabia ya wazazi kuwapeleka watoto wao nchini Kenya kwa ajili ya kupata elimu, huku wakiwataka wazazi kuwalinda mtoto wa kike na ndoa za utotoni ili kumuwezesha kupata elimu.
0 comments:
Post a Comment