Baraza la mazingira NEMC limekifungia
kiwanda cha wachina cha Group Six kilichopo mikocheni viwandani jijini Dar es Salaam
kinachojishughulisha na kazi za ujenzi ikiwemo kuchanganya zege,na kufyatua
tofali pamoja na faini ya milioni 60.
Kufungiwa kwa kiwanda hicho ni kutokana
na kuendesha shughuli zao bila kuwa na kibali cha NEMC na Osha.
Akizungumza na Tambarare Halisi mwanasheria
wa baraza la mazingira NEMC Bw.Heche suguta amesema kiwanda hicho kimekuwa
kikifanya shughuli zake za uzalishaji na kuathiri afya za wafanyakazi wa
kiwanda hicho pamoja na viwanda vingine kwa kutimua vumbi pia kiwanda hicho
kimekuwa kikisababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo na
kuwataka kufuata sheria za nchi na
kuaacha dharau kwa maofisa wa serikali.
Akiongea na maafisa hao mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho
ambaye hakutaka kutaja jina lake, ameonekana kutotambua mamlaka zinazotoa vibali nakusema wako katika
majaribio na kuonesha dharau kwa maafisa hao.
Naye mkaguzi wa majenzi kutoka Osha,mhandisi Swalehe Kasela
amelalamikia kuwepo kwa wawekezaji wasiofata sheria za nchi,kwa mujibu ya
sheria ya Osha ya mwaka 2003 inayomtaka mwekezaji kufika Osha mara tu anapokuwa
na wazo la kuanzisha kiwanda.
Nao wafanyakazi wa kiwanda hicho
ambao wameongea kwa mashrti ya kutopigwa picha kwa kulinnda ajira zao ,wamelalamikia
kutokuwepo kwa vifaa vya kufanyia kazi,na msilahi madogo ambyo hayalingani na
kazi ikiwa ni kulipwa ujira wa shilingi ishirini kwa kubeba tofali ambapo
wanatakiwa kubeba tofali mia 500 kwa siku.
Katika hali isiyo ya
kawaida,katika zoezi hilo Tambarare Halisi imegundua licha ya kuwepo kwa uzalishaji wa Zege na Tofali biashara
ya uuzaji wa vigae katika kiwanda hicho umekuwa ukifanyika,ambapo mwansheria wa
NEMC ameiomba serikali kufatilia kwa karibu kama biashara hiyo inalipiwa kodi.
0 comments:
Post a Comment