Timu ya Soka West Ham imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle katika mchezo wa ligi kuu ya England.
Kiungo
mfaransa Dimitri Payet ndio aliyepeleka majonzi kwa Newcastle baada ya
kufunga mabao mawili la kwanza dakika ya 9 kisha akaongeza bao la pili
dakika 48.
Newcastle United walitawala mchezo kwa asilimia kubwa
wakimiliki mchezo huo kwa asilimia 61 huku West Ham wakimiliki kwa
asilimia 39.
Kwa ushindi huo unawafanya wagonga nyundo hao wa
London kushika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 9
baada ya kucheza michezo mitano.
0 comments:
Post a Comment