Shirika la kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International limesema raia 380 wameuawa Kaskazini mwa Cameroon mwaka huu na wapiganaji wa Nigeria wa kikundi cha Boko Haram.
Katika ripoti yake mpya shirika hilo limesema pia kuna wanajeshi kadha waliouawa na wapiganaji hao ambao wamelazimisha watu 80,000 kukimbia makazi yao na maelfu ya wengine kuuawa.
Kwa upande mwingine wanajeshi na polisi wa Cameroon nao wanadaiwa kujibu mashambulio ya kundi hilo kwa kuwakamata zaidi ya watu 1,000, wengi wao wakiwa vijana.
Kulingana na shirika hilo lenye makao makuu yake huko London, Uingereza watu 200 waliokamatwa na maafisa wa usalama kwenye kilichoitwa operesheni Desemba kwa sasa hawajulikani waliko.

0 comments:
Post a Comment