Uingereza itajitolea wanajeshi kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kitakachopelekwa Sudan Kusini baada ya kutiwa saini mkataba wa kukomesha karibu miezi 20 ya mgogoro wa siasa wa nchi hiyo changa duniani.
Maelezo zaidi ya hatua hiyo ya Uingereza yatatolewa na Waziri Mkuu Bwana DAVID CAMERON wakati wa mkutano wa viongozi duniani utakaofanyika New York mwezi ujao ingawa mchango wa Uingereza kwenye vikosi vya kulinda amani duniani umekuwa mdogo sana.
Mwezi uliopita Rais SALVA KIIR wa Sudan Kusini na aliyekuwa naibu wake, ambaye sasa ni kiongozi wa waasi, Bwana RIEK MACHAR walitia saini mkataba wa amani wa kusitisha mapigano, ambayo yameua maelfu ya watu na kusababisha mamilioni ya wengine kukimbia makazi yao.
Mkataba huo ulitiwa saini kufuatia shinikizo la nchi za Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika na mataifa ya magharibi na Umoja wa Mataifa ambao umeonya kuwawekea vikwazo wote watakaojaribu kukiuka au kuvuruga utekelezaji wa mkataba huo.
Wakati huo huo mashirika ya masuala ya kibinadamu yanasema kumekuwa na mashambulio mengi ya wafanyakazi wa misaada huko Sudan ya Kusini ambapo 30 wameuawa tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuwepo matukio mengine ya kuibiwa na wafanyakazi wa misaada wanawake kuibiwa na kubakwa.
0 comments:
Post a Comment