Serikali ya Yemen inayoishi uhamishoni,ikiongozwa na Waziri Mkuu, Bwana KHALED BAHAH na mawaziri kadhaa imerejea nyumbani kutoka Saudi Arabia.
Msemaji wa serikali hiyo amesema Bwana BAHAH ambaye pia ni Makamu wa Rais na baraza lake la mawaziri watakaa mji wa bandari wa Aden.
Hatua hiyo inakuja baada majeshi yanayounga mkono serikali kuteka bandari hiyo kutoka kwa waasi wa kabila la Houthi ingawa haikujulikana mara moja kama Rais ABDRABBUH MANSOUR HADI pia atarejea.
Umoja wa Mataifa unasema watu wapatao 4,500 wakiwemo raia 2,110 wameuawa katika mapigano ya nchi kavu na mashambulio ya anga ya mseto unaoo9ngozwa na Saudi Arabia tangu Machi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment