Kampuni ya Apple ya Marekani imesema
kuwa ipo katika hatua za kukabiliana na shambulio la kimitandao,ambapo
wamebaini kuwa program hatari ya kimitandao iliyopo kwa watumiaji wa
simu za IPhone na iPad nchini China.
Watalaam wa ndani ya kampuni
hiyo wamesema kuwa inaelezwa kuwa hili ni moja la shambulio kubwa la
kimitandao kuwahi kuikumba kampuni hiyo.
Apple wanasema kwua
wavamizi hao wa kimitandao wanasema wamebuni namba za siri ambazo
huwawezesha watumiaji wa vifaa hivyo vya Apple kuingiziwa programu
zinazoathiri mawasiliano yao.
Msemaji wa Apple anasema kuwa
kampuni yao imeondoa kwenye mzunguko wa soko vifaa vyote vinavyotiliwa
shaka kuingiliwa na wavamizi hao wa kimitandao nchini China.
0 comments:
Post a Comment