Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, HALIMA DENDEGO amesema licha ya usafiri wa maji kutegemewa kwa kiwango kikubwa kusafrisha korosho,bandari ya mtwara bado inachangamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi ikiwemo kuongeza ghati za kuegesha meli.
Ametoa kauli hiyo wakati akizindua maonesho ya Siku ya Bahari Duniani ambayo kitaifa yanafanyika Mkoani Mtwara.
Amesema mbali na korosho bandari hiyo pia inategemewa kusafirisha saruji ambayo hivi punde itaanza kutengeneza kupitia kiwanda kikubwa cha saruji cha Dangote kilichopo mkoani humo.
Kufuatia changamoto hizo ametaka wadau kutumia maadhimisho hayo kutafakari njia sahihi zitakazotumika ili wafanyabiashara wanufaike, lakini pia Serikali kukusanya mapato.
Akizungumzia changamoto hizo mwakilishi wa meneja wa Bandari Mkoa wa Mtwara, MARK MUTAYOBA amesema serikali inatambua hilo na kupitia Mamlaka ya Bandari imetangaza zabuni ili ghati 4 za nyongeza zijengwe mwaka huu wa fedha 2015/2016.
Siku ya Bahari Duniani huadhimishwa Septemba 22 kila mwaka na mgeni rasmi hapo kesho anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dakta MOHAMED GHARIB BILAL.
0 comments:
Post a Comment