Image
Image

KENYATTA - Serikali yangu haina uwezo wa kuwalipa walimu.

Kenya imefunga shule zake za msingi na sekondari kutokana na mgomo wa walimu wanaodai nyongeza ya mishahara ya kati ya asilimia 50 na 60 .
Hata hiyo Wizara ya Elimu imeruhusu wanafunzi wa shule za juu za sekondari kuendelea na masomo katika kujiandaa na mitihani yao baadaye mwaka huu.
Akihutubia taifa Rais UHURU KENYATTA amesema serikali yake haina uwezo wa kuwalipa walimu nyongeza hiyo ya mishahara wanayodai kwani hivi sasa zaidi ya nusu ya mapato ya serikali yanatumika kwa mishahara ya watumishi wa umma.
Amewataka walimu kuwa  na huruma kwa watoto wa shule watakaoathirika kwa kurejea kazini na kukutana na serikali ili kufikia muafaka wa madai yao.
Mahakama ya Juu ya nchi hiyo imeunga mkono madai ya walimu hao wa Kenya wapatao laki tatu huku wapinzani wakijiandaa kwa maandamano wiki hii ya kuwaunga mkono walimu.
Hiki ndicho Uhuru Kenyata anacho sema juu ya Madai ya Walimu Tizama hapo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment