WAKAZI wa Jiji la Arusha wamekumbwa na hofu kubwa,baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa ni volcano kulipuka Mlima Meru.
Hali hiyo ilisababisha wingu zito la vumbi kutanda angani huku
wakazi wa vijiji vinavyozunguka mlima wakikimbia maeneo yao.
Wingu
hilo lililotanda angani lilianza kuonekana saa 9 alasiri upande wa
Kaskazini mwa Mlima Meru kisha kuendelea kusambaa hadi juu ya kilele cha
mlima huo.
Tambarare Halisi ilishuhudia vumbi hilo likielekea upande wa Kaskazini mwa
Jiji la Arusha kutokana na upepo uliokuwa ukivuma. Wakizungumza kwa
nyakati tofauti wakazi wa jijini hapa jana walionyesha wasiwasi na kudai
hawajawahi kuona vumbi zito likifunika mlima wote.
Kwa upande wake
mkazi wa Mianzini, Edward John, aliyeishuhudia hali hiyo alisema
inawezekana zikawadalili za kulipuka volcano.
“Najisikia kuvuta hewa nyepesi kifuani kama harufu ya saruji, vumbi linalotoka Mlima Meru,” alisema mkazi wa
eneo la Kaloleni, Lazaro Mtei.Vyanzo vya kutoka vijiji vya Kisimiri Juu na Ngarenanyuki, vilidai haikuwa volcano
kama ilivyohofiwa na watu wengi bali ni moto ulioanza kuwaka kwenye hifadhi ya mlima huo tangu juzi. Juhudi za
Kwa taarifa za muda huu ni kwamba mamlaka za hifadhi za mlima huo zimeelekea kuona ninamna gani yakudhibiti Volcano hiyo ambayo inaweza kuleta madhara makubwa kwa binadamu.

0 comments:
Post a Comment